Shalom!
Bwana Yesu apewe sifa!
Tuna kila sababu ya kumtukuza BWANA YESU kwa kutuwezesha kuumaliza mwezi wa tisa kwa ushindi na ushuhuda mkubwa. Kwa hakika tulikuwa na mwezi wa tisa mzuri ulioambatana na mfungo wa Danieli kwa siku 21. Ashukuriwe BWANA kwa kutu- wezesha kuwahudumia watu wake kiroho, kimwili, na kiakili ndani na nje ya Tanzania kwa mwezi wa tisa mwaka 2023. Katika kipindi hiki cha siku 21 za mfungo wa Danieli tumefanikiwa kufanya maombi, maombezi, ushauri na kutoa misaada mbalimbali pale ilipohitajika na kuwezekana. Kufanyika kwa haya yote si kwa uwezo wetu wala nguvu zetu bali ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu (Zekaria 4:6).
Disciples' Network
Think Act, Be Like Jesus.