Warumi 8:37
“Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda”.
Bwana Yesu apewe sifa!
Tunamshukuru Mungu ametuwezesha kushinda kwa kishindo, ndani ya mwezi Oktoba ambao ulikuwa ni mwezi wa ushindi wa vita vya kiroho na kimwili. Kwa msaada wa BWANA, tumeweza kuwahudumia watu wengi kiroho, kimwili, na kiakili ndani na nje ya Tanzania. Bila kuchoka wala kuzimia moyo, tumefanya maombi, maombezi, kutoa
ushauri na misaada mbalimbali pale ilipohitajika, kwa wote wenye uhitaji. Kuwezekana kwa haya yote ni kwa sababu BWANA yuko upande wetu, kutupigania na kutushindia (Warumi 8:37).
Disciples' Network
Think Act, Be Like Jesus.