Disciples' Network


Think Act, Be Like Jesus.

Category: Music

Disciples’ Network Praise & Worship Team-Mataifa (Official Song)


 

Wapendwa Disciples, tunayo furaha kubwa kuwaleta kwenu Praise and Worship team ya Disciple’s Network. Kipekee tunamshukuru Bwana Yesu Kristo aliyewawezesha kutengeneza nyimbo tatu kwa sasa, huu ukiwa ni mmoja wapo.

Uimbaji ni huduma ya kipekee sana. Nyimbo zinafikisha ujumbe, zinahubiri, zinafariji, zinatusaidia ktk kumuabudu na kumsifu Mungu na zinachangamsha. (moyo uliochangamka ni dawa, – Mithali 17:22)

Yeyote mwenye kipawa cha kuimba hatakiwi kukaa kimya, kwani kupitia wimbo wake kuna watu watapona, kufunguliwa au kutiwa moyo.

Je? wewe ni mwimbaji na unatamani kukuza kipawa chako? Au una karama au kipawa chochote hujaweza kuanza kukitumia? Karibu sana tushirikiane kukuza vipawa na karama kwa ajili ya kumtumikia Bwana Yesu Kristo.

Maandiko yanasema; Mwimbieni Bwana, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku. Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote. Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu. Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake. Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu. Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu; 1 Mambo ya Nyakati 16:23-29

Naomba uzidi kuwaombea Disciples Network praise team ili wazidi kusonga mbele ktk kuipeleka mbele injili.
Ubarikiwe sana.